Sunday, September 19, 2010

Nguo za Lesi

Lesi ni aina ya kitambaa kinachotengenezwa kwa kuvuta vuta kitambaa kupata kitambaa cha matundu matundu chenye umbile la kupendeza...lesi inaweza kutengenezwa kwa mashine ama mkono.....

Hii picha ya mwanzo kabisa Chantal amevaa nguo ya sketi nyeusi na blausi nyeusi ya lesikatika picha hiyo nyingine hii Chantal amevaa sketi nyeusi na blausi nyeupe iliyopitishwa lesi kwa juu...mfano imefumiwa....imependeza sana....na hii picha Mama Biya amevalia nguo ya lesi ya kizambarau iliyotulia na kofia ya misalaba maalum kwa ajili ya Papa...katika picha hii Madam amevaa nguo ya machungwa...na shati la lesi nyeusi...angalia jinsi nguo yake inavyotokeza kwenye shati la lesi nyekundu....ni nzuri mpaka basi....
Madam Chantal Biya anapenda sana kuvaa nguo za lesi....lesi ni kitambaa ambacho kinauzwa ghali sana madukani,na ukivaa nguo iliyotengenezwa na vitambaa hivi unapendeza sana,

katika picha hii Chantal amevaa nguo ya lesi ya kibuluu iliyotulia....amependeza sana

No comments:

Post a Comment